Mgogoro wa Syria umewasitisha shule watoto milioni 2: UNICEF

6 Septemba 2013

Takribani watoto milioni mbili nchini Syria wameacha shule au watoto karibu asilimia 40 walioandikishwa kati ya darasa la kwanza na la tisa wameacha masomo. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema karibu nusu ya watoto hawa wamekimbia machafuko na kuingia nchi jirani na wengi wao hawasomi. Jason Nyakundi na taarifa kamili

 (TAARIFA YA JASON NYAKUNDI)

UNICEF inasema kuwaSyriailikwa karibu kutimiza suala la elimu ya msingi kwa wote kabla ya kuanza kwa mzozo zaidi ya miezi miwili iliyopita. Wakati shule zinapotarajiwa kufunguliwa nchiniSyriana nchi majirani majuma machache yanayokuja hali inazidi kuwa ngumu zaidi. UNICEF inasema kuwa mfumo wa elimu ya umma nchini Lebanon una nafasi kwa wanafunzi 300,000 lakini serikali inakadiria kuwa   karibu watato 550,000 wenye umri wa kwenda shuleni kutoka Syria watakuwa nchini Lebanon ifikapo mwisho wa mwaka huu. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF

 (sauti ya Marixie)

 "Miezi thelathini tangu kuanza kwa mzozo , watoto wanaendelea kupatwa na mshangao. Tishio la kupotea kwa kizazi linazidi kuongezeka kila siku kwa kuwa hawako shuleni. Nchini Syria na eneo hilo lote, UNICEF inaunga mkono juhudi za kuwarejesha watoto kwenye masomo. UNICEF inaungno mkono kampeni za nchi nzima na shughuli za kusambaza bidhaa za masomo, kuwatafuta waalimu na kubuni madarasa ya kusomea.

Hata hivyo UNICEF inasema kuwa msaada wa kifedha unahitajika kuwahakikishia elimu watoto  nchini Syria.