Vijiji vyatelekezwa na kuna maelfu ya wakimbizi wa ndani Kaskazini CAR

6 Septemba 2013

Mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa Jamhuri ya Afrika ya Kati umearifu kwamba umebaini vijiji vilivyotelekezwa na maelfu ya watu waliotawanywa na machafuko ,ikiwa ni pamoja na ushahidi wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Umesema baadhi ya wanavijiji hivi sasa wanajificha msitumi, ripoti ya George Njogopa inafafanua zaidi.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Maafisa kutoka ofisi ya haki za binadamu waliokuwa wameambatana na wale wa shirika la kutoa misaada ya kiutu OCHA, walitembelea maeneo yaliyoko Kaskazini mwa Mji Mkuu wa Bangui na kushuhudia vitendo vinavyokwenda kinyume na misingi inayohimiza kuheshimiwa kwa haki za binadamu.

Katika taarifa yao, ujumbe huo umeorodhesha matukio kadhaa ikiwemo lile la kuchomwa moto kwa vijiji saba na kusababisha baadhi ya raia kukimbilia maeneo ya msituni kwa ajili ya kujificha wakihofia usalama wa maisha yao..

Kumekuwa pia na vitendo vya udhalalilushaji, watu kuteshwa ovyo na matukio ya kuwakamata raia bila sababu

Melissa Flemming ni msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR

(SAUTI YA MELISSA)