Guinea Bissau hali ni shwari, mamlaka ya mpito yafanya kazi: Ramos-Horta

5 Septemba 2013

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limepokea taarifa kuhusu hali ilivyo nchini Guinea-Bissau wakati huu ambapo wakazi wa nchi hiyo wanajiandaa kwa upigaji kura baadaye mwaka huu.

Mwakilishi maalum wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Jose Ramos-Horta akizungumza na waandishi wa habari baada ya mashauriano hayo ya faragha amesema amewaeleza wajumbe wa baraza hilo juu ya uwezekano wa uchaguzi mkuu wa tarehe 24 Novemba kuchelewa kidogo kutokana na ukata na vifaa vya uchaguzi.

Hata hivyo wajumbe wa baraza la usalama wameonyesha wasiwasi juu ya hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu, haki na ukwepaji sheria. Hata hivyo Bwana Ramos aliwatoa wasiwasi wajumbe..

(Sauti ya Ramos-Horta)

Nilikuwa na furaha kuweza kuwajuilsha kuwa Rais wa mpito atatuma barua kwa katibu Mkuu kuomba kuundwa kwa tume ya kimataifa ya kuchunguza vitendo vibaya vya uhalifu vilivyopita.”