Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za Nordic zaahidi dola milioni 750 kwa Global Fund

Nchi za Nordic zaahidi dola milioni 750 kwa Global Fund

Mfuko wa kimataifa wa kupambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria Global Fund umekaribisha kwa moyo mkunjufu ahadi ya dola milioni 750 iliyotolewa na nchi za Nordic ambao ni mchango mkubwa katika vita dhidi ya maradhi haya matatu.

Tangazo la ahadi hiyo limetolewa mjini Stockholm Septemba 4 kwenye taarifa ya pamoja ya nchi za Sweden ambaye ni mwenyeji , Norway, Finland, Denmark, Iceland na Marekani, sambamba na mkutano baina ya Rais Barack Obama na mwenyeji wake.

Kwa pamoja ahadi yao ni ongezeko la zaidi ya dola milioni 150 kutoka nchi za Nordic. Taarifa yao inasema mchango huo utafungua mlango wa ongezeko la dola milioni 375 kutoka Marekani . Mwenyekiti wa bodi ya Global Fund Dr Nafsiah Mbio amesema washirika wao wa nchi za Nordic muhimu saana katika kutokomeza maradhi ya ukimwi, kifua kikuu na malaria.