Vijana sasa wapatiwa tovuti ya kutoa maoni yao

5 Septemba 2013

Hii leo Mjumbe maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya vijana, Ahmad Alhendawi amezindua rasmi tovuti ambayo kwayo vijana watatumia kwa ajili ya kutoa maoni yaokuhusu masuala mbali mbali  yanayowahusu. tovuti hiyo  www.un.org/youthenvoy Katika mahojiano na radio ya  UM ameeleeza lengo la kuanzisha tovuti hiyo.

( SAUTI YA ALHENDAWI)

"Kile tunachojaribu kufanya tangu nianze hii kazi ni kuhakikisha tunatoa fursa kwa vijana kuungana na UM kwa kuweka taarifa zinazowahusu na fursa ndani ya mfumo wa UM katika sehemu moja. Kama unavyojua mfumo wa Umoja wa Mataifa ni mkubwa na wakati mwingine vijana wanachanganyikiwa wanapotafuta fursa au taarifa za maslahi tofauti katika maeneo mbali mbali , hivyo tunachojaribu kufanya ni kuweka eneo moja ambapo vijana wanaweza kupata taarifa kwenye mtandao moja un.org/youthenvoy ambako wanaweza kujifunza kuhusu mashirika ya UM yanayohusika na vijana na jinsi wanavyoweza kuchangia katika kazi za Umoja wa Mataifa."