Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awataka watu wa Maldives kuendesha uchaguzi ujao kwa amani na utulivu:

Ban awataka watu wa Maldives kuendesha uchaguzi ujao kwa amani na utulivu:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka watu wa Maldives kuhakikisha kwamba uchaguzi ujao wa Rais hapo Septemba 7 unafanyika kwa njia inayostahili na kwa amani.

Katika uchaguzi huo Ban amewachagiza wagombea wote wa Urais kuheshimu matokeo ya uchaguzi bila kujali nani ameshinda na amewataka wadau wote kumaliza tofauti zao.

Katibu Mkuu pia amewataka watu wote wa Maldives kushirikiana kujenga amani , utulivu wa kitaifa na demokrasia akigusia hususani haja ya ari ya mchakato wa kufanyia mabadiliko taasisi za kitaifa.