Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kesi ya Trayvon:Watalaam wa UM waitaka Marekani kukamilisha haraka uchunguzi wake

Kesi ya Trayvon:Watalaam wa UM waitaka Marekani kukamilisha haraka uchunguzi wake

Jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaoangazia watu wa asili ya Kiafrika wameitaka Marekani kukamilisha bila kuchelewa upitiwaji wa kesi ikiwemo mauwaji ya Trayvon Martin yaliyotokea February mwaka 2012.

Jopo hilo limetaka pia kutolewa kwa hukumu ya haki itakayokwenda sambamba na fidia kwa waathirika.

Idara ya Mahakama kwa kushirikiana na ofisi ya mwanasheria mkuu wa Jimbo la Florida imekuwa ikichunguza ushahidi wa serikali pamoja ili kuangalia uwezekano wa kuwepo kwa makosa yoyote katika kesi hiyo.

Kuuwawa kwa Trayvon Martin kulizusha hali ya taharuki na kufufua donda la ubaguzi wa rangi baada ya kijana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 17 kupigwa risasi na mlinzi George Zimmerman aliyedai alichukua hatua hiyo kama njia ya kujihami.