Watu 75,000 wakosa makazi Sudan Kusini

3 Septemba 2013

Mashirika ya kutoa misaada nchini Sudan Kusini yanasema kuwa hadi sasa yameandikisha kiasi cha watu 75,000 walioathiriwa na machafuko katika jimbo la Jonglei. 

Mashirika hayo yameanza kutoa huduma za usamaria wema ikiwemo usambazaji wa vyakula, maji pamoja na huduma nyingine za usafi.

(TAARIFA YA ALICE KARIUKI)

Shughuli za usambazaji wa misaada hiyo imeanza kwa kasi na tayari watu 55,000 wamefikiwa kwa kupatiwa huduma kama vyakula maji, na sehemu za kujihifadhi. Hata hivyo shughuli hizo za usambazaji wa misaada zinakumbana na hali ngumu kutokana na uchakavu wa bara bara hali inayofanya baadhi ya maeneo yasipitike kirahisi.

Mapigano yaliyozuka hivi karibuni baina ya vikosi vya serikali SPLA na kundi la waasi linaloongozwa na David Yau Yau yalisababisha idadi kubwa ya watu kukosa makazi na hivyo kuhitaji misaada ya kibinadamu.Pia kuzuka kwa mapigano ya makundi ya ndani baina ya lile Lou Nuer na Murle kuliongeza hali ya wasiwasi na kusababisha jamii nyingi kukosa misaada ya kiutu.

Yens Laerke ni msemaji wa OCHA:

 (SAUTI YA YENS LAERKE)