UNHCR yasema idadi ya wakimbizi wa Syria yafikia milioni mbili

3 Septemba 2013

Idadi ya wakimbizi wa Syria inaripotiwa kufikia milioni mbili wakati nchini Syria kwenye hali ikizidi kuwa mbaya kwa kuzalisha wakimbizi wa ndani.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kuwa hadi nchini Syria kwenyewe kuna zaidi ya wakimbizi 4.25. George Njogopa na maelezo kamili:

(PKG YA GEORGE NJOGOPA)

Kwa mujibu wa shirika hilo linasema kuwa kwa siku zaidi ya wakimbizi 5,000 hadi 6,000 hukatiza mipaka na kuingia katika nchi za jirani huku wakiwa watupu bila chochote mikononi mbali ya nguo chache wanazoondoka nazo.

Kamishna Mkuu wa UNHCR Antonio Guterres amesema kuwa uchungu na hali ngumu wanayokumbana nayo wananchi wa Syria kutokana na machafuko yanayoendelea yamezidisha kuwepo kwa maafa zaidi.

Amesema kadri maafa hayo yanavyozidi ndivyo yanavyosababisha ongezeko la wakimbizi katika nchi za jirani

Bwana Guterres amesema kuwa nchi zinazopokea wakimbizi wa Syria na kuwapa hifadhi zinahitaji msaada mkubwa kutoka jumuiya za kimataifa ili kukabiliana na mzigo unaowaandama

(SAUTI YA GUTERRES) ANDIKA PIA TUTAISOMA HUKU

“Kuhifadhi hali ya utengamao katika nchi zote katika kipindi hiki kigumu ni jambo la msingi mno. Vita tayari imeanza kusambaa hadi huko Lebanon, Iraq na kuna hatari ya kuvurugika kwa eneo ka Mashariki ya kati. Bila kuwepo kwa msaada wa hali na mali katika nchi hizi kama Lebanon, Jordan, na Iraq katika eneo la Kurdistan pamoja na Uturuki itakuwa ni vigumu mno kuleta ustamilivu katika nchi hizi na kushindwa kuzuia machafuko kuenea

Tumepanga kuona kiasi cha wakimbizi kikifikia milioni 3.5 hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, na hii inamaana kuwa tumejiandaa na hali kadhaa.