Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu yalaani vikali shambulio la Asharaf Iraq:

Ofisi ya haki za binadamu yalaani vikali shambulio la Asharaf Iraq:

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani vikali shambulio dhidi ya kambi ya Asharaf nchini Iraq siku ya Jumapili. Katika shambulio hilo wakaazi 47 wa kambi hiyo waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Ofisi ya haki za binadamu imeitaka serikali ya Iraq kuhakikisha ulinzi na usalama kwa wakazi wa kambi hiyo na kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya shambulio la Jumapili. Cécile Pouilly ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

 (SAUTI YA CECILE POUILY)

“ Tunaitolea wito serikali ya Iraq kuwahakikishia huduma za tiba haraka wale waliojeruhiwa na kuwahakikishia ulinzi wakazi waliosalia kambini Asharaf pia wale waqlioko katika kambi ya Liberty.”