Ugonjwa wa mabusha na matende waweza kumpata mtu yeyote

1 Septemba 2013

Ripoti ya shirika la afya ulimwenguni WHO, inasema kuwa zaidi ya  watu milioni 120 duniani kote wameathiriwa na ugonjwa huo wa mabusha na matende na  asilimia 65 ya watu hao wanaishi Kusini Mashariki mwaAsia, wakati asilimia 30 wako barani Afrika na idadi iliyosalia iko katika eneo la tropiki.

WHO inatoa mwito kwa nchi washirika kuongeza juhudi za kukabiliana na tatizo hilo ambalo bado halijapewa msukumo wa kutosha.Basi katika kipindi hikimaalum hii leo mwenzetu George Njogopa anaangalia hali ya ugonjwa huo nchini Tanzania na juhudi zinazochukuliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamiii. Karibu kuambatana naye.