Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban apewa taarifa na mkuu wa upokonyaji silaha kuhusu Syria:

Ban apewa taarifa na mkuu wa upokonyaji silaha kuhusu Syria:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo Jumamosi Agosti 31 amekutana na afisa wa Umoja wa mataifa wa masuala ya upokonyaji silaha Bi. Angela Kane ambaye ndio amerejea kutokaDamascuskwenye uchunguzi wa silaha za kemikali na kupewa taarifa ya kinachoendelea hivi sasaSyria.

Mkutano wao umefanyika wakati ambapo timu ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa ikiwasili Uholanzi mapema leo ili kufanya tathimini ya sampuli ilizokusanyaSyria. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky akizungumza na waandishi wa habari mjini New York amesema Bi Kane amempatia Bwana Ban taarifa kuhusu safari yake Syria na hali ya uchunguzi na ameishukuru serikali ya Syria na wapinzani kwa ushirikiano wao……

 (SAUTI YA MARTIN NESIRKY)

 Bi  Kane ametoa taarifa kwamba timu yao iliweza kufanya kufanya shughuli mbalimbali za uchunguzi kufuatia tukio la tarehe 21 Agost  kwenye eneo la Ghouta."

 Timu ya uchunguzi inaongozwa na mwanasayansiwa Sweden Dr.Åke Sellström, ambaye sasa yuko The Hague Uholanzi kwenye makao makuu ya shirika la kupinga sialaha za kemikali  (OPCW), akisaidia uchunguzi pamoja na shirika la afya duniani WHO. Nesirky akaendelea..

 (SAUTI YA NESIRKY)

“Mara tu baada ya timu kupata matokeo ya uchambuzi wa maabara wa sampuli , matokeo yake atafahamishwa bwana Ban ambaye anayasubiri kwa hamu  na haraka iwezekanavyo ili yaweze kuwasilishwa kwa wajumbe 193 nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na wale wa Baraza la usalama”

Bwana Ban anatarajia kupewa taarifa zaidi kesho Jumapili kutoka kwa Dkt. Sellström