Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serbia na Kosovo zapiga hatia katika kuboresha uhusiano

Serbia na Kosovo zapiga hatia katika kuboresha uhusiano

Viongozi kutoka mataifa ya Serbia na Kosovo wamepiga hatua  ambapo makubaliano ya kihistoria yameafikiwa kwenye jitihada za kuboresha uhusiano kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini Kosovo .

Akiwasilisha ripoti ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Kosovo Farid  Zarif ameliambia baraza la usalama kupitia kwa njia ya video kuwa  shuguhuli hiyo ni dhaifu na inahitaji uungwaji mkono na mwelekeo ulio imara.

Kati ya yale yaliyo kwenye makubaliano hayo yalitiwa saini mjini Brussels na mjumbe wa masuala ya kigeni kutoka kwa jumuiya ya ulaya Catherine Ashton na makubaliano ya kufanyika kwa uchaguzi mwaka huu mijini kaskazini mwa Kosovo.