Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wasio na vibali waliofukuzwa Tanzania kupatiwa misaada ya kibinadamu: IOM

Wahamiaji wasio na vibali waliofukuzwa Tanzania kupatiwa misaada ya kibinadamu: IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limesema liko kwenye washirika wake huko Tanzania,Rwanda na Burundi kuona jinsi ya kuwapatia misaada ya kibinadamu maelfu ya wakimbizi wasio na vibali ambao wameamriwa kuondokaTanzania ndani ya wiki mbili. Ripoti ya Jason Nyakundi inafafanua zaidi.

 (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Kupitia kwa amri ya rais wa Tanzania iliyotolewa tarehe 25 mwezi uliopita iliwaamrisha karibu wahamiji 35,000 kutoka Rwanda, Burundi na Uganda kuondoka nchini Tanzania ifikapo terehe 11 mwezi huu. Hadi sasa takriban  raia 13,000 kutoka Burundi, 7000 kutoka Burundi na 600 kutoka nchini Uganda wameitikia amri hiyo.

Wahamiaji wanawajumuisha wanawake wajawazito, watoto wasio na wazazi na watu waliolazimika kuhama makwao wakiwemo walio kwenye ndoa na wale wasiojua mwakwao ni wapi. IOM kupitia ushirikiano wa washirika kwenye huduma za kibinadamu ina mpango wa kuongoza kwa kuwapa misaada ya kibinadamu. Msaada wenyewe utajumuisha usajili na kubuniwa kwa vituo vya kupitia sehemu za mpaka ambapo wale wanaowasili watapata chakula, bidhaa zisizokuwa chakula na msaada wa matibabu. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM

(CLIP YA JUMBE OMARI JUMBE)

Kwa mujibu wa wizara inayoshughulikia masuala ya dharura na yale ya wakimbizi nchiniRwandani kwamba serikali tayari imeandaa vituo vitatu kwenye mpaka kuwahudumia raia wake wanaorudi nyumbani.