Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ASIA-PACIFIC iko mbioni kuwapa ajira kwa watu wa kipato cha wastani: ILO

ASIA-PACIFIC iko mbioni kuwapa ajira kwa watu wa kipato cha wastani: ILO

Shirika la kazi duniani ILO limesema ukuaji imara wa uchumi katika kanda ya Asia-Pacific kwa miongo miwili iliyopita kumesaidia kuwatoa mamilioni ya watu kwenye umasikini , huku ajira katika watu wa kiwango cha wastani ikiwa ni karibu 2/5 ya ajira yote ya kanda hiyo. Hata hivyo shirika hilo linasema ongezeko la ajira limekuja na ongezeko la kutokuwepo usawa pia.

Kwa mujibu wa ripoti ya karibuni ya ILO iliyochapishwa kwa jhina "ILO working paper" kuna zaidi wa wafanyakazi milioni 670 wa kiwango cha kati ambao wanaishi na familia zao kwa kiasi cha dola za Marekani 4 au zaidi kwa siku kwa mwaka 2012.

Idadi hiyo ni ongezeko la watu milioni 65 ikilinganishwa na mwaka 1991. Ukuaji wa ajira ya watu wa kiwango cha wastani imedhihirika zaidi Asia Mashariki ambako ongezeko limetocha chini ya asilimia 5 hadi zaidi ya asilimia 60 kwa kipindi cha miaka 20.