Hakuna utashi wa kisiasa kumaliza mzozo wa Syria kwa amani: IPU

30 Agosti 2013

Umoja wa mabunge duniani IPU umerejelea wito wake wa kutaka hatua za dharura zichukuliwe ili kumaliza mzozo unaoendelea nchini humo kwa amani, huku likieleza kuwa kinachokosekana ni utashi wa kisiasa. Ripoti ya George Njogopa inafafanua zaidi.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Rais wa IPU Abdel wahad Radi amesema kuwa hali yoyote ya mashambulizi ya kijeshi kutoka nje, kunaweza kusababisha maafa makubwa kuzidi yale yanayoshuhudiwa sasa ambayo yameshapoteza watu 100,000. Amesema kuwa Umoja wa mabunge umekaribisha hatua ya bunge la Uingereza lilikataa mpango ulipendekezwa na serikali ilitaka kuingia kijeshi nchiniSyria.

Bwana Abdelwahad amesema kuwa hatua hiyo iliyonyeshwa na bunge la Uingereza ni mfano tosha kwamba mabunge duniani kote yanauwezo wa kusaka  njia nyingine bora ya kusaka amani badala ya matumizi ya nguvu za kijeshi na uvurumishaji mabomu. Jemini Pandya ni msemaji wa IPU aliyeko Geneva

 (SAUTI YA JEMIN PANDYA)

“Tunaona kwa ukubwa kabisa kwamba muafaka wa kimataifa unaweza kufikiwa kwa njia ya kisiasa.Historia ya hivi karibuni inatuonyesha kuwa matumizi ya kijeshi siyo siyo njia sahii ya kufuatwa. Tayari kumekuwa na umwagaji mkubwa wa damu nchini Syria, nasi tunaamini kuwa hakuna haja ya kuendelea kufanya hivyo.Kile kinachokosekana ni kutokuwepo kwa utashi wa kisiasa ili kumaliza mzozo huu kwa njia ya amani na hiki ndicho kitu ambacho IPU inahisi kuwa kinalazimima kuwepo”

Bi Pandya amesema kuwa IPU inawasiliana kwa karibu na wabunge waSyria na iko tayari kutoa msaada wowote pindi itapohitajiwa.