Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa baraza kuu asisitiza haja ya mageuzi UM

Rais wa baraza kuu asisitiza haja ya mageuzi UM

Wakati Baraza  kuu la Umoja wa Mataifa likikutana kutathmini kile kinachoonekana juhudi za mabadiliko ya utendaji kazi, rais wa baraza hilo amezitolea mwito nchi wanachama kuhakikisha kuwa zinapigania mageuzi yanayomulika karne 21 ambayo ni utendaji wa pamoja .

Vuk Jeremic amesema kuwa nchi wanachama lazima zihakishe kwamba Umoja wa Mataifa unakuwa kitovu cha utendaji kazi wa pamoja katika dunia ya sasa.

Akizungumza na jopo la watendaji kazi wanaoangalia uwezekano wa kubadilisha mfumo wa Umoja wa Mataifa, rais huyo alizungumzia haja ya kulkiongezea uwezo baraza kuu.

Miongoni mwa mada zilizojadiliwa kwenye kikao hicho ni haja ya kuongeza idadi ya wanachama kwenye baraza la usalama.