Wataalamu wa nchi zisizopitiwa na bahari kukutana Geneva

30 Agosti 2013

Wataalamu wa usafiri kutoka nchi zilizoendelea ambazo hazijafikiwa na mkondo wa usafiri wa majini, wanatazamiwa kukutana Geneva kwa ajili ya kujadiliana namna ya ufanikishaji wa sera zitazoziwezesha nchi hizo kupata huduma ya usafiri wa bahari.

Mkutano huo uliopangwa kufanyika kuanzia Oktoba 22 hadi 24 ni maandalizi ya mkutano wa kimataifa utakaofanyika mwakani ambao utakuwa na kazi ya kutathmini miaka 10 ya mpango ujulikanao Programme of Action.

Mpango huo uliasisiwa mwaka 2004 ukiwa na lengo la kukabiliana na visingiti vinavyoziandama nchi zinazoendelea ambazo hazijafikiwa na mkondo wa bahari.

Kumekuwa na malalamiko kuwa nchi hizo zinaingia gharama kubwa kusafirisha bidhaa zao pindi zinapohitaji kutumia usafiri wa majini kupitia nchi zilizopitiwa na bahari.