Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID yazungumzia matokeo ya mkutano wa Arusha kuhusu amani Darfur

UNAMID yazungumzia matokeo ya mkutano wa Arusha kuhusu amani Darfur

Kaimu Mkuu wa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa huko Darfur, Sudan, Luteni Jenerali Wynjones Kisamba amesema mashauriano yaliyomalizika wiki hii huko Arusha kuhusu amani Darfur yametoa matumaini ya mwelekeo wa amani ya kudumu.

Katika mahojiano maalum na kituo hiki kutoka Sudan, amesema matumaini hayo ni kutokana na vikundi vikubwa ambavyo vilikuwa havijasaini makubaliano ya amani ya Doha kikiwemo kile cha Minni Minawi kushiriki mashauriano hayo yaliyoongozwa na Mkuu wa UNAMID Dkt. Mohamed Ibn Chambas.

(Sauti ya Lt. Jenerali Kisamba)