Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM kuendelea na operesheni zake Syria licha ya changamoto:

Mashirika ya UM kuendelea na operesheni zake Syria licha ya changamoto:

Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la mpango wa chakula WFP, la wakimbizi UNHCR, la kuhudumia watoto UNICEF, la afya WHO na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, yamesema yataendelea na operesheni zake mchini Syria licha la tishio la uvamizi wa kijeshi. Kwa mujibu wa mashirika hayo lengo ni kuwasaidia wakimbizi wa ndani na wakimbizi wengine licha ya changamoto wanazokabiliana nazo. Yameongeza kuwa kutokana na hali inayonendelea wafanyakazi wao wameelimishwa na kutakiwa kuchukua tahadhari.  Mashirika hayo yameongeza kuwa kwa sasa hayana mpango wowote wa kuondoa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kutoka nchiniSyria.