Ajali yaua watu 41 Kenya, WHO yataka hatua kuchukuliwa.

29 Agosti 2013

Watu 41 wameripotiwa kuaga dunia kwenye ajali mbaya ya barabarani iliyohusisha basi moja la abiria katika eneo la Ntulele lililo kwenye mkoa wa bonde laufanchiniKenyaambapo abiria wengine 33 walipata majeraha mabaya. Jason Nyakundi na taarifa zaidi.

(RIPOTI YA JASON)

Inaripotiwa kuwa basihilolililokuwa likiwasafirisha zaidi ya abiria 60 kutoka mji mkuu wa Kenya Nairobi likilekea mji wa Homabay ulio magharibi mwaKenyalilikosa mwelekeo na kupingira mara kadha saa chache baada ya usiku wa manane siku la Alhamisi. Watu 33 walifariki papo hapo huku wengine 8 wakifariki baadaye walipokuwa wakipata matibabu hospitalini. Watu wengine33 waliopata majeraha mabaya wanaendela kupata matibabu kwneye hosptali tofauti nchiniKenya. Akituma rambi rambi zake kwa familia za waathiriwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amasema kuwa hatua  amewataka madereva kuwa waangalifu na kuongeza kuwa hatua zitachukuliwa kuhakikisha maisha ya wakenya haipotei kwa ajali za barabarani.

(SAUTI RAIS KENYATTA)

Shirika la afya duniani WHO limesema limesikitishwa na ajali iliyotokea  Kenyana kuongeza kuwaKenya ni miongoni mwa nchi zenye sheria za usalama barabarani zinazohitaji kufanyiwa mabadili ili kulinda maisha ya wananchi na wasafiri kwa ujumla. Kilichosababisha kutokea kwa ajali hiyo hadi sasa hakijabainika.