Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko yazuka upya CAR na kusababisha mamia ya raia kukimbilia uhamishoni

Machafuko yazuka upya CAR na kusababisha mamia ya raia kukimbilia uhamishoni

Mapigano yaliyozuka upya katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Bangui yamesababisha zaidi ya watu 6,000 kukosa makazi na hivyo kuomba hifadhi ya muda.

George Njogopa na taarifa kamili:

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limearifu juu ya kuongezeka kwa mapigano hayo ambayo yameripitiwa zaidi katika eneo lijulikanalo Boy-Rabe na katika maeneo mengine ya jirani, yakihusisha vikosi vya serikali na wanamgambo.

UNHCR imeitaka serikali kuchukua hatua za haraka kuwalinda raia dhidi ya mashambulizi hayo na imetaka iwaruhusu kurejea majumbani mwao.

Taarifa zinasema kuwa wengi wa raia hao wameomba hifadhi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bangui na hivyo kuvuruga safari za ndege. Raia wengine wapatao 500 wanajihifadhi katika hospitali moja hatua ambayo imesababisha msongamano mkubwa wa watu na kuzusha kitisho cha kuzuka matatizo ya kiafya.

Babar Baloch ni msemaji wa UNHCR:

(SAUTI YA BABAR BALOCH) TAMKA BALOK NA ITAFSIRI PIA TUTAISOMA HUKU

“ Katika kipindi cha siku kumi zilizopita, kumekuwa na matukio ya kutiwa watu kizuiini, wengine wakiteswa na kukubwa na matukio ya uhalifu. Pia kumekuwa na ongezeko kubwa la matukio ya watu kupigwa ovyo jambo lililowalazimu raia wengi kukimbia makazi yao na hali hii inajitokeza katika maeneo yaliyoko jirana ya Boy-Rabe na Boeing maeneo ambayo yako Bangui.

Hali ya usalama ni mbaya na kwa raia inazidi kuwa mbaya siku baada ya siku.