Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na kuzungumza na viongozi Uholanzi, amani duniani yaangaziwa.

Ban akutana na kuzungumza na viongozi Uholanzi, amani duniani yaangaziwa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amekutana na kufanya mazungumzo na waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje wa Uholanzi katika tukio la maadhimisho ya miaka mia moja tangu ujenzi wa kasri la amani lililoko The Hague Uholanzi.

Katika mazungumzo yake na  waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte , viongozi hao wamaejadili maendeleo katika nchi za mashariki ya mbali, Syria, Misri, Mali na umuhimu wa ujenzi wa nchi na taasisi na kusaidia nchi hizi katika kipindi cha mpito pamoja na kugusia mageuzi ya Umoja wa Mataifa.

Katika mkutano na waziri wa mambo ya nje wa Uholanzi  Frans Timmermans Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alijikita katika mgogoro wa Syria na kazi ya timu ya uchunguzi wa silaha za kemikali . Pia walijadili juu yaMali, malengo ya maendeleo ya milenia na mkakati wa agenda za maendeleo baada ya 2015.

Kadhalika Bwana Ban ameishukuru Uholanzi kwa ushiriki wake katika operesheni za amani za Umoja wa Mataifa na kusisitiza uhitaji wa msaada zaidi wa vifaa kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA) hususani vifaa vya anga.