Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Askari mmoja wa kulinda amani wa UM auawa Goma, watatu wajeruhiwa

Askari mmoja wa kulinda amani wa UM auawa Goma, watatu wajeruhiwa

Umoja wa Mataifa umesema kuwa askari wake mmoja wa kulinda amani ameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa wakati wa operesheni ya kijeshi huko Goma Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Msemaji wa Umoja huo Farhan Haq amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa operesheni hiyo ya kijeshi iliyoanza Jumatano asubuhi inaendeshwa na jeshi la DRC dhidi ya waasi wa M23 kwenye eneo la Kibati ambalo waasi wamekuwa wakitumia kuanzisha mashambulizi dhidi ya raia.

Farhan amekariri ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu huko DRC, MONUSCO ukisema kuwa operesheni inaendelea.