Hatua zimepigwa katika utendaji wa jeshi la polisi Haiti:UM

28 Agosti 2013

Mwakilishi wa mpango wa Umoja wa mataifa nchini Haiti MINUSTAH Sandra Honore amesema kazi kubwa iliyofanywa na MINUSTAH nchini Haiti inatokana na uwajibikaji na ujuzi wa jeshi la polisi la nchi hiyo na polisi wa Umoja wa Mataifa UNPOL. Kwa pamoja wakishirikiana na serikali ya Haiti wameweza kuweka mpango wa maendeleo wa mwaka 2012 hadi 2016.

Akizungumza na radio ya Umoja wa Mataifa bi Honore amesema mpango ni kuhakikisha jeshi la polisi la Haiti linakuwa na askari 15,000 ifikapo 2015 na kuongeza kuwa kumekuwepo na hatua kubwa zilizopigwa katika kuboresha jeshi hilo japokuwa bado kuna kazi ya kufanywa.

Amesema bado kuna haja ya kuendelea kuimarisha uongozi wa polisi na kuwasambaza nchi nzima badala ya vituo vya mijini pekee.

(SAUTI YA SANDRA HONORE)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter