Watu wengi wajitokeza kupiga kwenye kambi ya Dadaab:UNHCR

28 Agosti 2013

Kwenye kambi yenye ukumbwa wa mji mdogo uchaguzi wa aina yake kuandaliwa  unaelekea ukingoni. Zaidi ya theluthi moja ya wakimbizi 400,00 wnaoishi kwenye kambi ya Daadab nchini Kenya wamejindikisha kuwapigia kura wagombea 1,002 waanowania uongozi tofauti huku kila nafasi ikiwania na mgombea wa kiume na kike. Flora Nducha na taarifa kamili

(RIPOTI YA FLORA NDUCHA)

Upigaji kura huo ulioanza siku ya Jumatatu ulifanyika kweye kambi tano za kambi kuu ya Dadaab na unatarajiwa kukamilika siku ya Alhamisi. Watu wengi wamekuwa wakikusanyika nje ya vituo vya kupigia kura kila siku  hali ambayo imesabaisha kuongezwa kwa saa za kupiga kura sehemu zingine ili kumpa kila mmoja fursa ya kushiriki.

Asilimia 60 ya wale walioasajiliwa tayari washapiga kura ambapo idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia 25 ikilinganishwa na zoezi la mwaka 2006. Sheikh sasa ana umri wa miaka 53 na ameishi kwenye ya Dadaab tangu mwaka 1991 baada ya kuikimbiaSomalia.

Anasema kuwa amefurahishwa na jinsi zoezihilolilivyoendeshwa akiongeza kuwa inamkumbusha miaka ya nyuma kabla ya mapinduzi yaliyofanyika nchiniSomalia. Patrick Musango ambaye ni mkuu wa idara inayohusika na masuala  ya wakimbizi kwenye kambi ya Dadaab anasema kuwa matarajioyaoni viongozi hao kusaidia katika kutekeleza masuala ya usalama na sheria. Emmanuel Nyabera ni msemaji wa UNHCR Kenya

(SAUTI YA NYABERA)