Shambulio lolote dhidi ya Syria liidhinishwe na Baraza la Usalama: Brahimi

28 Agosti 2013

Shambulio lolote la kijeshi dhidi yaSyriani lazima lipate idhini kutoka baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, amesema Lakhdar Brahimi, mwakilishi wa pamoja wa Umoja huo na Umoja wa nchi za kiarabu nchiniSyria. Ripoti ya Jason Nyakundi yafafanua zaidi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Akiongea mjini Geneva bwana Brahimi amesema kuwa anapinga hatua yoyote ya kijsehi kutoka nje akiongeza kuwa vita  kati ya wanajeshi wa serikali na makundi ya upinzani vimesababisha kuuawa kwa watu 100,000.Amesema kuwa kitu fulani kilitumiwa dhidi ya raia tarehe 21 mwezi huu mjini Damascus lakini pia akaongeza kuwa wachunguzi kutoka Umoja wa Mataifa walio eneo hilo ni lazima wapewe fursa ya kufanya uchunguzi wao

 (SAUTI YA LAKHDAR BRAHIMI)