Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wengi Tanzania wako hatarini kutokana na kujihusisha na uchimbaji wa madini

Watoto wengi Tanzania wako hatarini kutokana na kujihusisha na uchimbaji wa madini

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Watch Jumatano limechapisha ripoti inayoelezea mazingira magumu wanayokumbana nayo watoto wanaojiingiza kwenye ajira ya uchimbaji madini nchini Tanzania, jambo ambalo linakiuka mikataba ya kimataifa ya haki za watoto ukiwemo wa shirika la kazi ILO unaopinga ajira ya watoto, na kueleza kwamba wengi wa watoto hao wanakabiliwa na matatizo ya kiafya. Ripoti hiyo iliyotolewa jijini Dar es salaam inafuatia utafiti uliofanyika katika maeneo ya machimbo ambako watoto wengi wameajiriwa. George Njogopa anaarifu zaidi:

(Ripoti ya George Njogopa)