UNAMA imelaani vikali muaji ya wafanyakzi raia:

27 Agosti 2013

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa msaada Afghanistan UNAMA umelaani vikali vitendo vya karibuni vya utekaji na mauji ya raia sita kwenye jimbo la Herat. Miongoni mwa raia walionyongwa kulikuwepo wafanyakazi watato wa kamati ya kimataifa ya uokozi IRC shirika lisilo la kiserikali na mfanyakazi wa mpango wa kitaifa wa mshikamano.

IRC ni mshirika wa mpango wa kitaifa wa mshikamano, ambao ni mradi wa maendeleo wenye lengo la kuboresha maisha ya watu na kutoa fursa za kiuchumi kwa Waafghani wa kawaida wanaoishi katika jamii za vijijini nchi nzima. Kundi la Taliban limedai kuhusika na muaji hayo.

UNAMA imesema sheria za kibinadamu za kimataifa zinawataja raia kuwa ni wale wote ambao hawahusiki katika mapigano na ambao sio wanajeshi. Hivyo mashambulizi dhidi ya raia ni marufuku kwa wakato wowote ule na yanaweza kuwa ni uhalifu wa vita.UNAMA imetoa salamu za rambirambi kwa familia za wale wote waliouawa katika shambulio hilo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud