Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutimuliwa Wapalestina Ukingo wa Magharibi kuwaitia hofu ofisi ya haki za binadamu:

Kutimuliwa Wapalestina Ukingo wa Magharibi kuwaitia hofu ofisi ya haki za binadamu:

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kitendo cha kuondolewa na kuhamishwa kwa nguvu kwa Wapalestina kwenye Ukingo wa Magharibi ikiwemo Jerusalem Mashariki kinawatoa hofu. Hatua hiyo imetokana na bomoabomoa inayoendeshwa na uongozi wa Israel katika maeneo sita tofauti kuanzia tarehe 19 Agost mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya haki za binadamu iliyotolewa Jumanne , katika tukilo la Agost 19 uongozi wa Israel ulibomoa majengo katika jamii ya Mabedoin huko Tel al Adassa Mashariki mwa Jerusalem na kuziacha familia zote saba za takriban jumla ya watu 39 bila makazi na bila vibali vya majengo.

Uongozi wa Israel uliiamuru jamii hiyo kuondoka katika eneo hilo moja kwa moja au watakabiliwa na gharama kubwa za faini na kupokonywa mifugo yao .

Hakuna eneo au nyumba zozote za mbadala kwa watu hao zilizotengwa na hivyo kuwaacha katika mazingira ya sintofahamu.