Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNFPA yasema wanawake na wasichana wanapitia hali ngumu nchini Syria

UNFPA yasema wanawake na wasichana wanapitia hali ngumu nchini Syria

 Mfuko wa idadi ya watu wa Umoja wa Mataifa UNFPA umeelezea wasiwasi wake kutokaka na athari ambazo zimesababishwa na ghasia ndani na nje mwa mji wa Damascus nchini Syria hususan kwa wanawake, vijana na familia zao. UNFPA pia imeshangazwa na kuongezeka kwa ghasia zinaowalenga raia sehemu zingine za nchi hali ambayo imewalazimu idadi kubwa ya wanawake na wasichana kukimbilia usalama na kuingia kaskazini mwaIraq. Mkurugenzi mkuu wa UNFPA Babatunde Osotimehin anasema kuwa kile kinachostahili kueleweka ni kwamba wanawake , watoto na vijana nchiniSyriawameteseka vya kutosha. UNFPA pia inazikumbusha pande zinazozozana kuwahakikishia usalama wanawake na wasichana akiongeza kuwa UNFPA itaendela kuhakikisha kuwa kila mama aliye na mimba amelindwa, kila mtoto anayezaliwa yuko salama na ndoto ya kila kijana imetimizwa.