Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa mwongozo wa muda kutibu wagonjwa waliokumbwa na kemikali huko Syria

WHO yatoa mwongozo wa muda kutibu wagonjwa waliokumbwa na kemikali huko Syria

Shirika la afya duniani WHO hii leo limetangaza kuwa linatoa mwongozo wa muda wa tiba kwa wagonjwa waliokumbwa na kemikali nchini Syria. Mwongozo huo unazingatia mafunzo na maandalizi ambayo yamekuwa yakifanyika tangu mwaka 2012 kama anavyoripoti George Njogopa.

 (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA

Mwongozo huo mpya unatajwa kuwa ni wa aina yake kutokana na kujumuisha taarifa muhimu ambazo zinawabainisha wafanyakazi wa afya waliotumika kwenye maeneo hatarishi ikiwemo kukaa na wagonjwa waliopata maambukizi.

Ndani ya mwongozo huo kunakutikana taarifa zinazoanisha namna wahuudumu wanavyopaswa kuchukua tahadhari, hatua wanazopaswa kuzifuata kuwasaidia wale wagonjwa waliopata matatizo na madawa yanayopaswa kutumiwa.

Pia mwongozo huo umeweka jedwari linaloelezea mtitiriko wa hatua zinazopaswa kufuata wakati wa utoaji huduma za kitabibu.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari Msemaji wa WHO  Glen Thomas alisema kuwa, kutolewa kwa mwongozo huo hakujafungamano na tukio la kutumwa waangalizi wa Umoja wa Mataifa huko Syria ambao wanaendesha uchunguzi kuhusiana na kutumika kwa silaha za kemikali katika moja ya mashambulizi ya hivi karibuni.

(SAUTI YA GLEN THOMAS).