Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO yazindua nyenzo kupiga vita dhidi ya ajira ya watoto:

ILO yazindua nyenzo kupiga vita dhidi ya ajira ya watoto:

Shirika la kazi duniani ILO limezindua mafunzo ya muongozo wa hatua za kuongeza vita dhidi ya mifumo mibaya ya ajira ya watoto. Kwa mujibu wa ILO nyenzo hiyo mpya ina lenga kuchagiza juhudi za muongozo kuelekea lengo la kutokomeza mifumo mibaya ya ajira ya watoto ifikapo mwaka 2016.

Muongozo huo umeainisha maana ya mifumo mibaya ya ajira ya watoto na kuwasilisha mikakati ya kuitokomeza. Pia imeelezea mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa na serikali, wafanyakazi na mashirika mengine ya kijamii kukabiliana na tatizo hilo.