Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya UM kuhusu haki za watoto yasikitishwa na mauaji ya kutumia silaha za kemikali:

Kamati ya UM kuhusu haki za watoto yasikitishwa na mauaji ya kutumia silaha za kemikali:

Kamati ya Umoja wa mataifa ya haki za watoto imesema madai ya shambulio la silaha za kemikali kwenye viunga vya Damascus Syria lililo katili maisha ya watu zaidi ya 300 wakiwemo watoto ni zahama na mfano wa kutisha wa jisni watoto wanavyolipa gharama ya vita nchiniSyria. Jason Nyakundi na maelezo kamili

(TAARIFA YA JASON NYAKUNDI)

Mwenyekiti wa kamati hiyo Kirsten Sandberg amesema kuwa vitendo hivyo ni ukiukaji mkubwa wa haki za watoto akiongeza kuwa ni jambo la kushangza kuona jinsi haki za watoto zinavyokiukwa wakati mzozo waSyria unavyozidi kuwa mbaya zaidi.

Amesema kuwa wowote waliohusika kwenye mauaji hayo na uhalifu mwingine dhidi ya watoto nchini Syria lazima watafikishwa mbele ya sheria. Bi Sandberg amesema kuwa mkataba kuhusu haki ya mtoto unatumika wakati wote akiongeza kuwa zaidi ya watoto 7000 wameuawa tangu kuanza kwa mzozo na wengine wengi kujeruhiwa.

Kamati hiyo inaungana kwenye wito kutoka kwa tume ya haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa kwa kuzitaka pande zote husika  kukoma kulenga raia. Mwaka 2011 wakati wa kukaguliwa  kwa makataba huo kamati husika iliorodhesha baadhi ya ukiukaji wa haki za binadamu ambao umefanyiwa watoto nchini Syria zikiwemo haki za kuishi  , usalama na mateso.