Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msafara wa wachunguzi wa UM kuhusu matumizi ya silaha za kemikali washambukliwa

Msafara wa wachunguzi wa UM kuhusu matumizi ya silaha za kemikali washambukliwa

Syria, taarifa zinasema walenga shabaha wa kuvizia wameufyatulia risasi msafara wa wakaguzi wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukielekea kwenye eneo linaloshukiwa kuwa na silaha za kemikali. Assumpta Massoi na taarifa kamili

(TAARIFA YA ASSUMPTA MASSOI)

Gari ya kwanza ya wakaguzi hao wa silaha za kemikali lifyatuliwa risasi makusudi mara kadhaa na watu wasiojulikana katika eneo la amani.Na kwa kuwa risasi hizo zimeharibu gari , timu ya wakaguzi imerejea salama kwenye kituo cha serikali cha ukaguzi na inatarajiwa kurejea kwenye eneo hilo baada ya kubadilisha gari. Umoja wa Mataifa umesisitiza kwamba kila upande lazima uonyeshe ushirikiano ili kwamba timu hiyo iweze kufanya kazi yao kwa usalama.

Wakati huohuo Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema dunia haitomudu kuchelewa zaidi kutopata ufumbuzi wa madai ya matumizi ya silaha za kemikali.

Akizungumza mjini Seoul Korea ya Kusini  amesisitiza kuwa kila dunia nzima imeshuhudia kwenye runinga picha za kutisha za tukio hilo hivyo ni muhimu familia zikapata majibu na serikali ya Syriai na wajibu wa kupata ukweli.

(SAUTI YA BAN)

"Sisi sote tumeona picha, hakika hili ni tukio kubwa na la kutisha, tunawajibika kwa familia za wahanga.Wale wote wako Syria wana wajibu wa kupata ukweli. Dunia nzima inapaswa kuwa na wasiwasi juu ya tishio lolote au matumizi ya silaha za kemikali. Ninatoa amri kuwa pande zote ziruhusu ujumbe huu kuanza kazi yake ili tuweze kuanza kujua ukweli wa mambo."