Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkakati wa usafi wa mikono ni muhimu kwa afya:WHO

Mkakati wa usafi wa mikono ni muhimu kwa afya:WHO

Shirika la afya duniani WHO limesema mkakati wa kuimarisha usafi wa mikono ni rahisi kwa wahudumu wa afya kuutekeleza kwa mujibu wa utafiti mpya uliochapishwa Ijumaa na jarida la afya la Uingereza Lancet. Flora Nducha na taarifa kamili

 (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Kwa mujibu wa WHO utafiti huo mpya ni kuhusu magonjwa ya kuambukiza kupitia wahudumu wa afya.

WHO imeongeza  kuwa maambukizi yanayohusishwa na huduma ya afya ni tishio kubwa kwa usalama wa wagonjwa duniani na maambukizo hutokea kupitia mikono ya wahudumu wa afya.

Tarik Jasarevic ni msemaji wa , WHO anasema utafiti huo uliohusisha nchi sita  ikiwamo , Costa-rica naMali, umeonyesha mafanikio.

 (SAUTI YA TARIK JASAREVIC)