Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mgogoro wa Syria ni tishio kubwa kwa amani na usalama wa duniani: Brahimi

Mgogoro wa Syria ni tishio kubwa kwa amani na usalama wa duniani: Brahimi

Mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na jumuiya za a nchi za kiarabu Lakhdar Brahimi ameeelezeaa hofu iliyopo kutokana na madai ya kutumika kwa silaha za kemikali mjini Damascus nchini Syria. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(Taarifa ya Jason)

Akiongea mjini Geneva bwana Brahimi amesema kuwa tukio hilo ni ishara ya hatari ambayo haiwaandami watu wa Syria bali eneo hilo lote na dunia nzima. Mjumbe huyo amesema kuwa ikiwa pande zinazo zozana zitashikilia msimamo kuwa mzozo uliopo utasuluhishwa kwa njia ya kijeshi, hali itazidi kuwa mbaya zaidi akiongeza kuwa majadiliano ndiyo suluhisho tu  kwa kuwa hali iliyo sasa ni tishio kwa amani na usalama wa dunia nzima.

 (Sauti ya Brahimi)

 Tatizo ni kwamba pande zinazohusika kwenye vita hivi kila mmoja inafikiri kuwa itashinda kwa njia ya kijeshi. Tunaamini,  katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na watu wengine wengi wanaamini kuwa hakuna suluhu la kijeshi, hakuna upande utashinda. Na kuna  suluhu tu la kisisa na vile tunavyofanya mapema ndivyo itakuwa sawa. Kwa sasa Syria ndiyo tisho kubwa kwa amani na usalama duniani. Kile kinachofanyika sasa na habari hizi za matumizi ya silaha za kemikali na uharibifu wa nchi ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka miwili , wakati tatizo hilo likiendelea kuenea nje mwa Syria, kupitia kuhama kwa wakimbizi na kuhusika kwa nchi majirani wa njia moja au nyingine kwenye mzozo, ndilo kwa sasa tisho kubwa kwa amani na usalama.”

(Sauti ya Brahimi)

Brahimi anasema kuwa barabara ya kuelekea kwa suluhu la kisiasa tayari imewekwa kwenye mkutano ulioandaliwa mjiniGenevatarehe 30 mwezi Juni.