Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP bado inahitaji dola milioni 84 kuwasidia watu wa Sudan Kusini

WFP bado inahitaji dola milioni 84 kuwasidia watu wa Sudan Kusini

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema nchini Sudan Kusini linawasaidia watu milioni 1.7 lakini bado linahitaji dola milioni 84 ili kuweza kupanua wigo wa msaada wao kuwafikia watu takribani milioni 2.85 wanaohitaji msaada.

Kiwango hicho cha fedha kinajumuisha dola milioni 20 ombi kwa ajili ya Jonglei pamoja na kulipa madeni ambayo yanaisaidia serikali kupeleka chakula vijijini kabla ya msimu wa mvua ambazo ni kiasi cha dola milioni 29. Mbali ya msaada wa chakula WFP inaziwezesha jamii kukabiliana na mafuriko, ukame na majanga mengine ya asili na yake yanayochangiwa na binadamu.