Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msukumo wa kufikia malengo ya milenia ni haki na muhimu:Ban

Msukumo wa kufikia malengo ya milenia ni haki na muhimu:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ambaye yuko ziaranai nchini Korea Kusini amesema msukumo wa kufikia malengo ya maendeleo ya milenia MDG’s ni muhimu na ni haki.

Ban ameyasema hayo alipokutana na mabalozi mbalimbali mjini Seoul na kuongeza kuwa bara la Afrika limepiga hatua kubwa kimaendeleo kupitia utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia hususani katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi, malaria na kifua kikuu lakini akatoa angalizo kwamba licha ya hatua hizo bado umaskini njaa pamoja na tishio la amani na usalama ni changamoto barani humo

 (SAUTI YA BAN)

 "Lengo la kimataiafa la kupunguza nusu ya umaskini lilitimizwa mwak 2010 lakini kiwango cha umaskini bado kinabakia kuwa juu sana, kikizidishwa na kukuwa kwa tofauti kati ya na miongonbi mwa nchi za Afrika . Njaa inasalia kikwazo kisichokubalika katika kufikia utu wa binadamu. Ninasumbuliwa sana na muendelezo wa ukosefu wa chakula na upungufu lishe hususani kwa watoto na wanawake wajawazito . "