Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM imepanua huduma za usafiri kwa wakimbizi wa Syria:

IOM imepanua huduma za usafiri kwa wakimbizi wa Syria:

Shirika la Kimataifa linalohusika na uhamiaji IOM limechukua hatua ya kupanua huduma za usaifiri ili kuwakirimu mamia wa wakimbizi wa  Syria ambao idadiyaoinazidi kuongezeka nchiniIraq.

Ripoti zinaonyesha kuwa idadi ya wakimbizi wanaongia nchini humo imeongezeka katika siku za hivi karibuni na hadi sasa IOM inasema kuwa imesafirisha wakimbizi wengine 32,000 wakipitia maeneo ya Sahela na Peshkhabour. Ongezeko hilo linatajwa kuwa kubwa zaidi tangu kuzuka kwa mzozo huo wa Syria miaka miwili iliyopita.