Ban awa na mazungumzo na Rais Park wa Korea Kusini

23 Agosti 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye yupo ziarani Korea ya Kusini leo amekutana na mwenyeji wake Rais Park Geun-hye na kisha kujadiliana masuala mbalimbali yakiwemo yale yanayohusu ushirikiano. 

Ban alipongeza Korea Kusini jinsi ilivyo mstari wa mbele kushiriki kwenye majukumu ya kimataifa pamoja na kwamba taifa hilo siyo mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama.

Alisema Korea imetoa mchango mkubwa katika maeneo yanayohusu ulinzi wa amani, mabadiliko ya tabia nchi pamoja na agenda ya maendeleo endelevu.

Ama viongozi wote wawili wamekubaliana kuendelea kuwapiga jeki kwa misaada ya kibinadamu mamia ya raia wa eneo hilo ambao wanakabiliwa na matizo mbalimbali.