Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Myanmar yasonga mbele lakini ishughulikie chuki za kidini

Myanmar yasonga mbele lakini ishughulikie chuki za kidini

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya  haki za binadamu nchini Myanmar, Tomás Ojea Quintana, amesema nchi hiyo imepiga hatua katika maeneo mengi jambo lililoleta mabadiliko chanya katika hali ya haki za binadamu lakini bado kuna changamoto katika suala la chuki za kidini. Taarifa zaidi na Joseph Msami.

 (Taarifa ya Joseph Msami)

Akiongea baada ya kukamilisha ziara yake ya nane nchini Myanmar, mtaalamu huyo hata hivyo ameonya kuhusu changamoto zilizosalia ikiwamo uhitaji wa upatanisho wa makundi ya kikabila na kusambaa kwa uchochezi wa chuki baina ya makundi madogo ya kidini.

Bwana Quintana amesema serikali inapaswa kutimiza wajibu wake kwa kuzuia kuenea kwa chuki za kidini, kuanzishwa kwa utawala wa kisheria na kutekeleza sera za viwango vya kimataifa vya  haki za binadamu.

"Myanmar imekuwa katika migogoro inayohusisha silaha kwa miongo kadhaa , changamoto ya serikalia ni kuanza kuchukua hatua katika ngazi ya shina ili machakato huu uwe jumuishi na makundi madogo na makabila yana sauti katika machakato huu wasikiklizwe, ushiriki wa wanawake pia ni muhimu. Bila ushiriki  halisi wajamii za makundi ya kikabila hili litachukua muda mrefu na matarajaio ya mafanikio kuwa magumu zaidi."

Jaribio la mtaalamu huyo maalum wa UM kuzuru eneo liitwalo Meiktila ambapo mapigano yaliyolenga jamii za kiislamu yalisababisha watu zaidi ya elfu kumi kujkosa makazi , 43 kufariki liligonga mwamba baada ya waandamanaji kuvamia gari lake.