WHO yaidhinisha dawa mpya ya kutibu mabusha na matende

22 Agosti 2013

Shirika la afya duniani WHO limeridhia matumizi ya dawa ya kutibu magonjwa yaliyosahaulika hususan mabusha na matende, magonjwa yaliyo tishio hasa kwenye nchi za kitropiki ikiwemo Afrika. Ripoti  ya George Njogopa inafafanua zaidi.

 (Taarifa ya George)

Dawa hiyo aina ya NTD002 inayozalishwa na kampuni ya Eisai ya nchiniJapanitatumikakamakinga dhidi ya ugonjwa wa mabusha na matende ambao kwa miaka mingi umeachwa bila kutiliwa mkazo. Katika hatua yake ya kwanza, kampuni hiyo imehaidi kuipatia WHO kiasi cha  vidonge bilioni 2.2 ikiwa ni shabaha mahususi ya kutokomeza kabisa tatizo hilo.

WHO imesema kuwa imekubali kupokea dawa hizo kutokana na kile ilichokiita kukithi viwango vya kimataifa na ikayataka makampuni mengine kuiga mfano ulionyeshwa na Eisai kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora wa viwango.

Zaidi ya watu milioni 120 wameathiriwa na ugonjwa huo wa mabusha na matende na  asilimia 65 ya watu hao wanaishi Kusin Mashariki mwaAsia, wakati asilimia 30 wako barani Afrika na idadi iliyosalia iko katika eneo la tropiki.