Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huenda kuchelewa kwa mvua kukaathiri mavuno nchini Mali:WFP

Huenda kuchelewa kwa mvua kukaathiri mavuno nchini Mali:WFP

Msimu wa mvua nchini nchini Mali umeanza ukiwa umechelewa hali ambayo huenda ikaathiri pia mavuno. Taifa la Mali linajaribu kujikwamua kutoka kweye mzozo uliosababisha kuhama kwa watu wengi na tatizo la ukosefu wa chakula mwaka 2011. Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linawasidia wakulima eneo la Segaou umbali wa kilomita 200 kaskazi mashariki mwa mji mkuu Bamako. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Nchini Mali msimu wa mvua mara nyingi huanza mwezi Mei na kuendelea hadi mwezi Oktoba. Mvua hizo huchangia kukua kwa vyakula kama mtama na huwa na umuhimu kwa kilimo cha mchele. Hali imekuwa hivi kwa karne nyingi lakini kwa miaka michache iliyopita kila kitu kimebadilika. Msimu wa mvua wa mwaka 2011- 2012 haukuwa mzuri sawia na mavuno. Watu walio kusini hawakuwa na nafaka ya kutosha hali ambayo iliathiri taifa zima kutokana na kuwepo ukosefu wa bidhaa za kuuza. Muda mfupi baada ya kuanza kwa mzozo, kuhama kwa watu kulisababisha kuwepo ukosefu mkubwa wa bidhaa hizo. Kando na oparesheni zake zikiwemo za usambasaji wa chakula na kuwapa fedha wakimbizi wa ndani Shirika la mpango wa chakula duniani linawasaidia watu na mahitaji muhimu . Mamadou Togola afisa kutoka WFP nchini Mali anasema kuwa kwa sasa kile ambacho watu wa Mali wanahitaji ni mavuno mazuri lakini sasa mvua zimeanza zikiwa zimechelewa.