UNHCR yakaribisha azimio la nchi za Asia-Pacific linalolenga kukabili wahamiaji haramu

UNHCR yakaribisha azimio la nchi za Asia-Pacific linalolenga kukabili wahamiaji haramu

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limekaribisha hatua ya nchi za ukanda wa Asia-Pasific ambazo zimeahidi kukabiliana na wimbi la uhamiaji haramu unaosababisha mamia ya watu kupoteza maisha kila mwaka wakati wakiwa baharini.

Kauli hiyo ya UNHCR imekuja baada ya kumalizika kwa mkutano wa siku moja uliofanyika katika mji mkuu wa Indonesia Jakarta ambao pia uliwahisisha maafisa kutoka nchi zote za eneo hilo na ale wa shirika la kimataifa la uhamiaji.

Mkutano huo umeidhinisha azimio la pamoja ambalo limeanisha hatua za kukabiliana na tatizo hilo la wasafiri haramu.Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kuweka mifumo sahihi ya kiutendaji ambayo itasaidia kuainisha sheria za uhamiaji.