Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa na tuhuma za matumizi ya kemikali leo Damascus

Ban asikitishwa na tuhuma za matumizi ya kemikali leo Damascus

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amestushwa na tuhuma za matumizi ya silaha za kemikali leo  katika vitongoji mjini Damascus Syria.

Katika taarifa yake aliyoitoa mjini New York Bwana Ban amesema atahakikisha uchunguzi wa kina wa tuhuma zilizowasilishwa katika ofisi yake.

Tuhuma hizi zinakuja wakati huu ambapo timu ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza tuhuma za matumizi ya silaha za kemikali inayoongozwa na Professor Åke Sellström iko nchini Syria. Uchunguzi huo unafuatia madai yaliyowasilishwa kwa Umoja wa Mataifa  na nchi wanachama.