Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA kuzisaidia nchi za Sahel kusaka maji ya ardhini:

IAEA kuzisaidia nchi za Sahel kusaka maji ya ardhini:

Katika bara la Afrika eneo la Sahel ndio kame zaidi duniani na nchi zilizo katika eneo hilo zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa maji huku watu wakitegemea maji ya ardhini na mahitaji ynaongezeka. Sasa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA linashirikiana na nchi za Sahel ili kubaini uwepo wa maji ardhini katika kanda hiyo kwa kutumia njia ijulikanayo kama “Isotope Hydrology”.

Kwa njia hiyo wanasayansi wanaweza kubaini kiasi, ubora na uwezo wa kujaa maji hayo. Eric J Cole ni afisa wa mpango huo wa IAEA kwa Sahel , anaelezea hatua zilizopigwa katika mradi huo wa Sahel.

(CLIP YA ERIC J COLE)