Bara la Afrika huenda likakabiliwa na ukosefu wa chakula ikiwa hatua hazitachukuliwa:UNEP

21 Agosti 2013

Kutokana na kuwepo kwa mabadadiliko ya hali ya hewa kuna hofu kwamba bara la afrika huenda likakabiliwa na changamoto za ukosefu wa chakula ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa. Inakadiriwa kuwa kati ta mataifa kumi yaliyo maskini zaidi duniani na yanayokabiliwa na tatizo la ukosefu wa chakula manane kati yao yako kwenye bara la Afrika. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

RIPOTI YA JASON

Mkutano ulioandaliwa kwenye makao ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi Kenya uliwaleta pamoja wataalamu kutoka nchi tofauti za bara la Afrika na waakilishi kutoka kwa mashirika ya Umoja wa Mataiafa ambao wamejadiliana mbinu ambazo zinaweza kulikomboa bara la Afrika kutokana na tatizo la kutokuwepo chakula cha kutosha wakati amnbapo dunia inaposhuhudia mabadiliko ya hali ya hewa. Richard Munang ni mratibu wa masuala mabadiliko ya hali ya hewa kwenye Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataiffa Kanda ya Afrika.