Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yaimarisha doria jimboni Pibor

UNMISS yaimarisha doria jimboni Pibor

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, umeanzisha doria ya kijeshi katika jimbo la Pibor ili kuimarisha usalama katika eneo hilo na mji wa Gumuruk hatua itakayowezesha wananchi kurejea makwao na pia kuwezesha ugawaji wa misaada ya chakula.

Kwa mujibu wa taarifa ya UNMISS, doria hiyo huendeshwa kila siku kwa kutumia magari na kutembea kwa miguu ambapo walinda amani hutumia fursa hiyo kuwatambua waathirika wa mapigano ya hivi karibuni, pamoja na kuzungumza nao kwa lengo la kukusanya taarifa za hali ilivyo jimboni Pibor kuhusu hali za raia na zoezi la ugawaji wa chakula

Katika zoezi hilo ambalo hadi sasa limeshayafikia maeneo ya umbali wa kilometre 18 UNMISS inasema imepata ushirikiano mkubwa kutoka serikalini, vikosi vyenye silaha na mamlaka jimboni humo.