Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaingiwa hofu juu ya umaskini na ukosefu wa uhakika wa chakula Misri

WFP yaingiwa hofu juu ya umaskini na ukosefu wa uhakika wa chakula Misri

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema lina hofu juu ya ongezeko la umaskini na ukosefu wa uhakika wa chakula nchini Misri hususan miongoni mwa jamii maskini wakati huu ambapo mzozo wa kisiasa unazidi kushamiri na hali ya uchumi ikidorora. Grace Kaneiya na taarifa kamili.

 (Taarifa ya Grace Kaneiya)

WFP imesema kuwa itaendelea kufuatilia hali ya mambo kwa karibu n wakati huo huo inaendelea kupokea taarifa zinazoelezea hali jumla ilivyo kwenye eneo hilo.

Licha ya kukabiliwa na mikwamo ya hapa na pale, WFP iliendelea na jukumu lake la usambazaji wa misaada ya chakula katika kipindi cha mwezi Julai na August.

Ndani ya mwaka huu 2013,zaidi ya Misri 650,000 wanatazamiwa kunufaika na miradi inayoendeshwa na WFP. Katika kipindi cha mwezi Julai wakimbizi  wapatao 35,000 wa syrian waliripotiwa kuweka kambi nchini Misri.

Na ndani ya mwezi huu wa August WFP imepanga kuwafikia zaidi ya wakimbizi 50,000.